Kunguni-maji

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kunguni-maji
Remove ads

Kunguni-maji ni wadudu wadogo hadi wakubwa wa oda za chini Gerromorpha na Nepomorpha katika oda Hemiptera ya nusungeli Pterygota (wenye mabawa) ambao huishi majini. Mabawa yao ya mbele ni nusu magumu na nusu kama viwambo. Kunguni hao hula wadudu wengine ama hai au waliokufa, na spishi kubwa hula samaki na amfibia wadogo pia.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Mifano ya wadudu hao ni wendamaji na kunguni-bahari (familia Gerridae), wapima maji (Hydrometridae), nge-maji (Nepidae), waogeleaji-juuchini (Notonectidae), kunguni-makasia (Corixidae), kunguni-maji wakubwa (Belostomatidae), kunguni-maji watambaazi (Naucoridae), kunguni-chura (Gelastocoridae)

Remove ads

Biolojia

Kundi la kunguni-maji lina spishi ndogo sana (mm 2) na spishi kubwa sana (sm 12) zilizomo miongoni mwa wadudu wakubwa kabisa duniani. Spishi za Gerromorpha hutembea juu ya maji au huishi katika mahali panyevu, lakini zile za Nepomorpha huogelea chini ya maji kwa kawaida.

Takriban spishi zote ni mbuai wa wadudu wengine na spishi kubwa vilevile mbuai wa samaki na amfibia wadogo, lakini hula mizoga pia. Spishi nyingine hula mimea ya majini au dutu za mimea. Sehemu za kinywa zina umbo la kutoboa mbuawa ili kufyonza damu yake. Spishi fulani, kama nge-maji na kunguni-makasia, zinaweza kutoboa ngozi ya watu na kuuma sana.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads