Mpima maji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wapima maji ni wadudu wadogo wa familia Hydrometridae katika oda ya chini Gerromorpha ya oda Hemiptera wanaofanana na kijiti kidogo kana kwamba kupima maji. Spishi nyingi hutembea juu ya maji sehemu ya wakati, lakini nyingine huishi katika mahali panyevu, hata ndani ya mapango. Jenasi 2 zinatokea Afrika: Heterocleptes na Hydrometra.
Remove ads
Maelezo
Wapima maji wana urefu wa mm 3-22[1]. Wana mwili uliorefuka na mwembamba sana, haswa spishi za jenasi Hydrometra, ambazo kichwa chao ni takriban theluthi moja ya urefu wa mwili na vipapasio vinaweza kukaribia nusu ya urefu wa mwili. Spishi zote zina miguu mirefu na sehemu za kinywa ndefu zinazoweza kupenya. Spishi nyingi hazina mabawa, ingawa baadhi zina mabawa. Wana rangi ya kijivu au kahawia.
Biolojia
Wadudu hawa ni wa kawaida kiasi na wamepatikana duniani kote. Tofauti kubwa zaidi, hata hivyo, inapatikana ndani ya ukanda wa tropiki na Hydrometra pekee inatokea mahali pengine. Kwa kawaida hutokea kwenye nyuso za maji kwenye kingo za maziwa, mabwawa na maeneo oevu, mara nyingi ambapo samaki hawapo. Wanapendelea uoto wa majini au wanatembea polepole kwenye maji tulivu, lakini watasogea haraka wakisumbuliwa[2]. Wako mbuai na watajilisha kwa wadudu wanaoishi juu ya maji, wadudu mkia-fyatuo wakiwa mojawapo ya milo wanayopenda zaidi. Pia hufyonza wadudu walioanguka ndani ya maji. Spishi nyingi kiasi huishi katika maeneo yenye unyevunyevu, baadhi katika mapango. Wote ni wapandaji wakubwa na hupanda mimea kutafuta wadudu wa kula. Hutumia kinywa chao chenye ndaka ili kupenya mbuawa wao na kuingiza mate. Kisha hufyonza tishu zilizokuwa kiowevu[3].
Mayai hutagwa kwenye mashina ya mimea. Kwa ujumla wamegundulika kuwa na hatua tano ya lava na kuwa wapevu ndani ya wiki nne hadi sita.
Remove ads
Spishi kadhaa za Afrika
|
|
Picha
- Hydrometra australis
- Hydrometra gracilenta
- Hydrometra stagnorum akifyonza kiowevu cha mdudu mkia-fyatuo
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads