Habakuki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Habakuki alikuwa nabii wa Israeli ya Kale aliyeishi na kufanya kazi wakati mmoja na nabii Yeremia (karne ya 7 KK).

Mbele ya uovu na ukatili wa binadamu alitabiri hukumu ya Mungu, lakini pia huruma yake[1].
Hababuki aliandika kitabu kifupi ambamo alithubutu kumuuliza Mwenyezi Mungu kwa nini anaadhibu Israeli vikali kwa mikono ya watu wabaya kuliko wao.
Jibu ni kwamba Mwenyezi Mungu ana njia zake ambazo anaandaa ushindi wa haki: hivyo mwadilifu ataishi kwa imani yake (1:12-2:4).
Usemi huo ukaja kutumika sana katika Agano Jipya. Mtume Paulo ameufanya msingi wa msimamo wake kuwa wokovu unapatikana kwa imani, si kwa kujitahidi kutekeleza masharti yote ya Torati.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads