Henri II

From Wikipedia, the free encyclopedia

Henri II
Remove ads

Henri II (6 Mei 972 13 Julai 1024) alikuwa kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma tangu tarehe 7 Juni 1002 hadi tarehe 13 Julai 1024.

Thumb
Kaisari Henri II.

Ni kaisari pekee wa Ujerumani aliyetangazwa kuwa mtakatifu. Ilitokea mnamo Julai 1147 kwa tamko la Papa Klementi II.

Sikukuu yake ni tarehe 13 Julai[1].

Ndoa yake na maisha ya kiroho

Mke wake, Kunegunda wa Luxemburg, akaja pia kutangazwa mtakatifu na Papa Inosenti III mwaka 1200. Ilisadikiwa kwamba hawakuzaa watoto kutokana na uamuzi wao wa kuishi katika ndoa kama kaka na dada kwa sababu za kidini[2].

Hakika Henri alijiunga kiroho na Wabenedikto kama mtawa wa nje.

Pamoja na mkewe alishughulikia sana ustawi wa Kanisa Katoliki katika dola lake kwa kutetea haki za maaskofu na kuhimiza uaminifu wa mapadri kwa useja mtakatifu uliowapasa. Vilevile alijitahidi kueneza imani ya Kikristo kote Ulaya. Kwa ari hiyo ya kimisionari alianzisha majimbo mengi na monasteri.

Thumb
Henri II akitiwa taji la Kaisari.
Thumb
Kaburi la Henri na Kunegunda lililotengenezwa na Tilman Riemenschneider.
Thumb
Ukurasa wa Thietmar's Chronicle.
Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads