Isaka Mkuu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Isaka Mkuu (pia: Sahak Partev; 354 hivi - Bagrevand, 439) alikuwa mmonaki, mwanateolojia na askofu kutoka Armenia ya Kale.

Mtoto wa Nerses I na kilembwekeza wa Gregori Mletamwanga, alipofiwa mke wake alijiunga na monasteri, halafu kama Patriarki alipigania umoja wa Kanisa kwa msingi wa imani sahihi ya Mtaguso wa Efeso, lakini akaja kufukuzwa jimboni akafariki uhamishoni.
Pia alisaidiana na Mesrop kutafsiri Biblia na alirekebisha liturujia na sheria za Kanisa[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Septemba[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads