Mesrop
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mesrop Mashtots (pia Mesrob Mashtotz, kwa Kiarmenia Մեսրոպ Մաշտոց; Hatsik, Armenia ya Kale, leo nchini Uturuki, 361 hivi - Wagharshapat, Armenia, 17 Februari 440) alikuwa mmonaki, mwanateolojia, mshairi na mtaalamu wa lugha mwanafunzi wa Patriarki Nerses I.



Anaitwa "Mwalimu wa Armenia" kwa kuwa ndiye aliyebuni alfabeti ya Kiarmenia (406) ili waamini waweze kujua Biblia ya Kikristo akaitafsiri yote akaanzisha shule nyingi akiweka hivyo misingi ya taifa hilo na ustaarabu wake uliolidumisha hata leo kati ya matatizo makubwa ya historia yake, hasa dhuluma za kidini [2].
Baada ya kufanya kazi ikulu, alipata daraja takatifu na kujiunga na umonaki akaanzisha mtindo wa monasteri kuwa na shule karibu nayo ili kuandaa watu watakaoendeleza elimu ya dini hasa kwa kutafsiri na kunakili vitabu.
Mapema monasteri kubwa zikawa pia na seminari kuu au vyuo vikuu vya teolojia.
Hivyo umonaki wa Armenia ulidumisha utamaduni wa taifa hilo, ambalo lilikuwa la kwanza kupokea Ukristo jumla pamoja na mfalme wake (300) halafu likaushika moja kwa moja hata lilipopitia vipindi vigumu sana.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Filamu
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads