Jimbo Kuu la Songea

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jimbo Kuu la Songea
Remove ads

Jimbo Kuu la Songea (kwa Kilatini Archidioecesis Songeana) ni mojawapo kati ya majimbo makuu 7 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, likiongoza majimbo ya kusini, yakiwemo Mbinga, Tunduru-Masasi, Mtwara, Lindi na Njombe.

Kama majimbo yote 36 ya Kanisa Katoliki nchini, linafuata mapokeo ya Kiroma.

Makao makuu ni mjini Songea, ambapo pana Kanisa kuu la mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba.

Askofu mkuu ni Damian Denis Dallu tangu tarehe 14 Machi 2014.

Remove ads

Takwimu (mwaka 2004)

Jimbo lenyewe la Songea lina waamini 223.111 (46.9%) kati ya wakazi 476.161 wa eneo lote la kilometa mraba 38,600.

Mapadri ni 105, ambao kati yao 62 ni wanajimbo na 43 watawa. Hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia Wakatoliki 2,124 katika parokia 27.

Pia jimboni wanaishi mabruda 227 na masista 458.

Historia

Baada ya hatua mbalimbali ya uinjilishaji chini ya wamonaki Wabenedikto, tarehe 6 Februari 1969 jimbo liliundwa rasmi, halafu tarehe 18 Novemba 1987 lilifanywa jimbo kuu kwa hati Christi Domini ya Papa Yohane Paulo II.

Maaskofu

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Kuu la Songea kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads