Kalimantan

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kalimantan
Remove ads

Kalimantan (inajulikana pia kwa jina la Borneo ya Indonesia) ni sehemu kubwa ya kisiwa cha Borneo iliyopo Indonesia.[1] Sehemu hii ni asilimia 73 za eneo lote la kisiwa hicho. Sehemu nyingine zisizo za Indonesia ni Brunei na Malaysia ya Mashariki.

Thumb
Ramani ya Kalimantan na sehemu zake

Etimolojia

Jina la Kalimantan (pia Klemantan) linatokana na lugha ya {{Kisanskrit]]: Kalamanthana ikimaanisha kisiwa chenye hali ya hewa joto sana. Linafanywa na maneno mawili: kal(a) (wakati. majira) na manthan(a) (moto sana, ya kuchoma). [2]

Eneo

Sehemu hii ya Indonesia ina asilimia 73 (km² 544,150 [3]) za kisiwa chote cha Borneo na 69.5% (watu 13,772,543 wakati wa sensa ya 2010) za wakazi wa kisiwa hiki. Sehemu zisizo za Kiindonesia ni Brunei (wakazi 400,000) na Malaysia ya Mashariki (wakazi 5,625,000) inayokumlisha majimbo ya Sabah, Sarawak na eneo la Labuan.

Utawala

Kalimantan ina mikoa 5 :

Maelezo zaidi Mkoa, Eneo(km2) ...

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads