Kartaki wa Lismore

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kartaki wa Lismore
Remove ads

Kartaki wa Lismore (pia: Mo Chutu, Mochuda, Kartaki Kijana; Fingen, Ireland, 555 hivi - Lismore, Ireland, 14 Mei 639[1]) alikuwa padri aliyekwenda kuishi upwekeni miaka 14, halafu akajiunga na monasteri ya Bangor kabla ya kuanzisha ya kwake huko Rathin akiipatia kanuni mpya kwa lugha ya Kieire.

Thumb
Mtakatifu Kartaki pamoja na Katerina wa Aleksandria na Patrik wa Ireland.

Mwaka 635 yeye na wanafunzi wake walifukuzwa huko na hatimaye akawa askofu wa kwanza wa Lismore[2] baada ya kuanzisha huko monasteri nyingine iliyovuta vilevile wafuasi wengi[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi[4] na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 14 Mei[5].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads