Kiguudau
Ndege wa maji wa familia Heliornithidae From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Viguudau ni ndege wa maji wa familia Heliornithidae. Familia hii ina spishi tatu tu, kila moja katika jenasi yake. Ndege hawa wana mwili mwembamba, shingo ndefu, mkia mpana na domo lenye ncha kali. Wana tando za ngozi kati ya vidole vyao zinazowasaidia kuogelea. Wanatokea kanda za tropiki kwa maji yatiririkayo polepole au katika vinamasi na mabwawa ya mikoko. Hula wadudu, makoa, gegereka, vyura na samaki wadogo. Hujenga tago lao la vitawi na mimea kwa matete.
Remove ads
Spishi ya Afrika
- Podica senegalensis, Kiguudau wa Afrika (African finfoot)
Spishi za mabara mengine
- Heliopais personatus (Masked finfoot)
- Heliornis fulica (Sungrebe)
Picha
- Kiguudau wa Afrika
- Masked finfoot
- Sungrebe
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads