Mkoko

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoko
Remove ads

Mikoko ni aina za miti au vichaka vinavyokua katika maji ya chumvi kwenye fuko za bahari za kanda za tropiki[1]. Miti hii inaainishwa katika jenasi tatu: Bruguiera, Ceriops na Rhizophora katika familia Rhizophoraceae. Pengine jina hili hutumika kwa Theobroma cacao lakini afadhali jina mkakao litumike kwa mti huu.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Takriban 1/3 ya pwani kwenye tropiki huwa na mikoko au miti ingine inayoweza kukua katika maji ya chumvi[2]. Msitu wa mikoko huitwa kapa au wangwa.

Mizizi ya mikoko inaweza kushika matope na hivyo husaidia kukinga pwani na kujenga visiwa.

Remove ads

Spishi za Afrika

  • Bruguiera gymnorhiza, Mchofi, Mkoko Wimbi, Mshinzi, Msindi, Msinzi au Mui (Black mangrove)
  • Ceriops tagal, Mkandaa au Mkoko Mkandala (Indian mangrove)
  • Rhizophora mangle, Mkoko Mwekundu Magharibi (Red mangrove)
  • Rhizophora mucronata, Mkoko Magondi au Mkoko Mwekundu Mashariki (Asiatic mangrove)

Spishi za mabara mengine

Remove ads

Picha

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads