Kitabu cha Ruthu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kitabu cha Ruthu ni kimojawapo kati ya vitabu vifupi vya Biblia ya Kiebrania, kwa hiyo pia ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Ni kati ya vile vichache vilivyo na jina la mwanamke ambaye ndiye mhusika mkuu wa habari.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Remove ads
Umuhimu wake
Katika fujo ya miaka ya Waamuzi (Kitabu cha Waamuzi), habari ya kitabu hiki kifupi inatujenga: inamhusu Ruthu, mwanamke Mpagani wa kabila la Moabu aliyeolewa na Mwisraeli kwao, ng’ambo ya mto Yordani.
Baada ya kufiwa mume wake akafuatana na mama mkwe Naomi hadi Bethlehemu ili aolewe na ndugu wa marehemu na kumzalia mtoto kadiri ya Torati, sheria ya Israeli.
Baada ya kufanikiwa kuolewa na Boazi kwa msaada wa Naomi, alimzaa Obedi.
Huyo mtoto akawa baba wa Yese na babu wa mfalme Daudi.
Hivyo kwa uaminifu wake mwanamke huyo pia akatajwa katika Injili kama bibi wa Yesu (Math 1:5-6).
Remove ads
Mazingira
Habari kuu ya kitabu cha Ruthu ilitokea wakati wa Waamuzi, lakini inafurahisha moyo, ikilinganishwa na hali mbaya ya kidini na ya kimaadili iliyoandikwa katika kitabu cha Waamuzi.
Habari yenyewe inaonyesha kwamba imani kamili kwa Mungu na uangalifu na upendo kwa watu wengine wakati ule pia ulikuwepo katika Israeli.
Katika taifa zima walikuwepo watu waliojitahidi kuishi maisha ya unyenyekevu na haki mbele ya Mungu wa kweli.
Habari hiyo pia inaonyesha kwamba Mungu aliwaangalia watu kama hao kwa neema yake kubwa, akiyaongoza mambo yao ya kila siku na kuwafanikisha. Wema huo pia ulikuwa baraka kwa taifa zima.
Remove ads
Yaliyomo
- 1:1-22 Miaka kumi ya taabu katika nchi ya Moabu
- 2:1-4:22 Mwanzo wa maisha mapya katika Israeli
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads