Kodivaa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kodivaa
Remove ads

Kodivaa[1] (kwa Kifaransa: Côte d'Ivoire[tanbihi 1], rasmi Jamhuri ya Kodivaa ni nchi ya Afrika ya Magharibi. Imepakana na Liberia na Guinea upande wa magharibi, Mali na Burkina Faso kaskazini, Ghana mashariki na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki upande wa kusini. Ikiwa na idadi ya watu milioni 32 ni nchi ya 32 kubwa duniani kwa idadi ya watu. Yamoussoukro ndio mji mkuu na Abidjan ndio mji mkubwa.

Ukweli wa haraka Jamhuri ya Kodivaa République de Côte d'Ivoire (Kifaransa), Mji mkuu ...
Remove ads
Thumb
Abidjan ni mji mkubwa na muhimu zaidi kiuchumi wa Ivory Coast .
Remove ads

Historia

Baada ya uhuru (7 Agosti 1960) iliwahi kuwa kati ya nchi tajiri zaidi za Afrika lakini tangu mwaka 2002 uchumi na hali ya maisha kwa jumla vimeharibika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe (2002-2011).

Watu

Wakazi walikadiriwa kuwa 29,344,847 mwaka 2023, lakini sensa ya mwaka huo ilihesabu idadi ndogo zaidi: 29,389,150.

Kabila kubwa ni lile la Waakan (38%). Asilimia 22% ni wahamiaji, hasa kutoka nchi jirani (Liberia, Burkina Faso na Guinea). Asilimia 4 wana asili tofauti, hasa Ufaransa, Lebanoni, Vietnam na Hispania.

Lugha zinazotumika kawaida ni 68, lakini lugha rasmi ni Kifaransa.

Upande wa dini, Uislamu una 42.5%, Ukristo 39.8% (Kanisa Katoliki peke yake 24.9%), dini asilia za Kiafrika 2.2% na dini nyingine 0.5%. Wasio na dini ni 12.6%

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

  1. Tamka: kot divwar. Jina la Kifaransa lina maana ya "pwani ya pembe za ndovu"

Marejeo

Loading content...

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads