Konklevu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Konklevu
Remove ads

Konklevu (kutoka Kilatini "cum clave", yaani "kwa ufunguo", kupitia matamshi ya Kiingereza ya neno "conclave") ni mkutano maalumu ya makardinali wote wenye umri chini ya miaka 80 unaofanyika ili kumchagua askofu wa Roma, maarufu kama Papa wa Kanisa Katoliki, baada ya kufariki dunia au kujiuzulu aliyekuwa madarakani.

Thumb
Moshi mweusi kutoka Kikanisa cha Sisto IV ni ishara ya kwamba Papa mpya hajachaguliwa.[1]
Thumb
Moshi mweupe ni ishara ya kwamba Papa mpya amechaguliwa.[1]

Lengo la kujifungia ndani tangu karne za kati ni kuzuia makardinali wasiingiliwe na watu wa nje, hasa watawala, ambao wanaweza wakawa na malengo tofauti na yale ya kiroho.

Kwa sasa kuna taratibu nyingi zilizopangwa kinaganaga, ambazo mojawapo ni kwamba wapigakura wasizidi 120, ingawa Papa ana mamlaka ya kuzidisha.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads