Kosta Rika
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kosta Rika, rasmi kama Jamhuri ya Kosta Rika (kwa Kihispania: República de Costa Rica), ni nchi ya Amerika ya Kati inayopakana na Nikaragua kaskazini, Panama kusini, Bahari ya Karibi mashariki, na Bahari ya Pasifiki magharibi. Ina idadi ya watu takriban milioni 5, na ni ya 126 duniani kwa ukubwa wa eneo. Mji wake mkuu na mkubwa zaidi ni San Jose. Kosta Rika inajulikana kwa utulivu wa kisiasa, mfumo wa kijamii wa maendeleo, na juhudi zake za uhifadhi wa mazingira, ikiwa ni miongoni mwa nchi zenye viwango vya juu vya maisha na uhifadhi wa maliasili katika ukanda huo.

Kosta Rika ilikuwa nchi ya kwanza duniani ya kufuta jeshi lake kikatiba. Pia inaongoza kwa kuhifadhi mazingira.
Costa Rica, rasmi kama Jamhuri ya Costa Rica, ni nchi katika Amerika ya Kati, inapakana na Nicaragua kaskazini, Panama kusini mashariki, Bahari ya Pasifiki magharibi, na Bahari ya Karibea mashariki. Ina idadi ya watu takriban milioni 5.2, ikiwa ya 120 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni San José, ambalo pia ni mji mkuu. Costa Rica inajulikana kwa utulivu wa kisiasa, bioanuwai tajiri, na kujitolea kwa uhifadhi wa mazingira.
Remove ads
Historia
Kabla ya kufika kwa Wahispania katika karne ya 16, nchi ilikaliwa na Waindio wachache.
Mwaka 1821 koloni hilo lilijiunga na ghasia ya maeneo mengine ya Amerika ya Kati dhidi ya utawala wa Hispania.
Mwanzoni nchi hizo ndogo zilijiunga na Meksiko lakini baada ya miaka miwili zilianzisha "Shirikisho la Amerika ya Kati" lililokwisha mwaka 1839.
Tangu mwaka 1847 Kosta Rika imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.
Mwaka 1948 kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo viliwahi kwisha. Mwaka uliofuata nchi ilifuta kabisa jeshi hadi leo[1][2][3].
Remove ads
Watu
Wakazi wengi (65.8%) wana asili ya Ulaya, mbali ya machotara Wazungu-Waindio (13.65%) na wahamiaji wenye asili yoyote (9.03%). Waindio, ambao ndio wakazi asili, ni 2.4% tu.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania.
Upande va dini, walio wengi ni wafuasi wa Yesu katika Kanisa Katoliki (70.5%: ndiyo dini rasmi) au madhehebu ya Uprotestanti (13.08%). Nje ya Ukristo, unaongoza Ubuddha (2.3%).
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads