Laurenti Huong Van Nguyen

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Laurenti Huong Van Nguyen (1802 hivi - 27 Aprili 1856) alikuwa padri wa Vietnam aliyekamatwa usiku alipokwenda kumhudumia mgonjwa mahututi. Kwa kuwa alikataa kukanyaga msalaba, aliteswa na hatimaye akakatwa kichwa chini ya kaisari Tu Duc. [1].

Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads