Leobini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Leobini
Remove ads

Leobini (kwa Kifaransa: Lutiti; Poitou, karne ya 5 - Chartres, 14 Machi 557[1]) alikuwa askofu wa mji huo, leo nchini Ufaransa, katikati ya karne ya 6[2].

Thumb
Sanamu yake huko Louviers.

Baada ya kuchunga mifugo na kulima alijifunza kusoma akajiunga na monasteri, lakini wakati mwingine aliishi kama mkaapweke. Pia aliteswa na Wafaranki. Hatimaye akawa shemasi na abati kabla ya kufanywa askofu mwaka 544[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Machi[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads