Leufridi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Leufridi
Remove ads

Leufridi (pia: Leutfridus, Leutfrido, Leufredo, Leutfrid, Leufroi, au Leufroy; alifariki Evreux, 738[1]) alikuwa mmonaki Mbenedikto wa Ufaransa, ndugu wa mtakatifu Agofredus na mwanafunzi wa mtakatifu Sidoni wa Saint-Saëns.

Thumb
Sanamu yake katika kanisa lililojengwa kwa heshima yake.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Juni[2].

Maisha

Leufridi alisoma katika abasia ya Condat na huko Chartres, akawa kwa muda fulani mwalimu huko Evreux.

Baada ya kuishi kama mkaapweke sehemu mbili tofauti, alianzisha monasteri ya La Croix-Saint-Qu'en mwaka 690 hivi, akawa abati wake wa kwanza na kuliongoza kwa miaka 48 hivi.[1][3]

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads