Lugha za Khoisan

From Wikipedia, the free encyclopedia

Lugha za Khoisan
Remove ads

Lugha za Khoisan ni lugha za Afrika ambazo ni maalumu kwa fonimu zake nyingi sana (hadi 141), kuliko lugha nyingine zote duniani.

Thumb
Uenezi wa lugha za Khoisan barani Afrika (rangi ya njano).
Thumb
Lugha za Kikhoe-Kwadi na nyingine kati ya kundi la awali la Kikhoisan.

Zimeenea hasa Kusini mwa Afrika, lakini zinatumika pia katika wilaya ya Chemba, mkoa wa Dodoma, Tanzania ya kati.[1]

Hii inaonyesha kwamba kabla ya uenezi wa makabila ya Kibantu, lugha hizo zilitawala barani Afrika kusini kwa ikweta.

Baadhi ya lugha hizo zimeshakufa na nyingine ziko hatarini. Karibu zote hazina maandishi.

Ile inayotumiwa na watu wengi zaidi (250,000 hivi) inaitwa Khoekhoe ("Nàmá") na inapatikana nchini Namibia. Inafuatwa na Kisandawe nchini Tanzania (40,000-80,000).

Hata hivyo siku hizi wataalamu wanakusha uwepo wa kundi hilo kubwa kwa sababu wanaona tofauti kati ya lugha hizo ni kubwa mno.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads