Mkoa wa Dodoma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mkoa wa Dodoma, mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania, uko katikati ya nchi ukipakana na mikoa ya Manyara, Morogoro, Iringa na Singida. Kutokana na nafasi hiyo, mji mkuu wa mkoa umefanywa mji mkuu wa nchi pia. Jiji la Dodoma lina bunge la Tanzania na chuo kikuu kikubwa zaidi nchini. Eneo lote la mkoa ni la km² 41,310. Sehemu kubwa ni nyanda za juu kati ya mita 830 hadi 2000 juu ya UB. Mkoani kuna uzalishaji mkubwa wa divai, unaoongoza barani baada tu ya Afrika Kusini. Katika sensa ya mwaka 2022, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ilihesabiwa kuwa 3,085,625. [1]



Kuna wilaya nane zifuatazo: Bahi, Chamwino, Chemba, Dodoma Mjini, Kondoa, Kondoa Mjini, Kongwa, Mpwapwa. Wilaya ya awali ya Dodoma Vijijini imegawiwa katika wilaya mpya za Chamwino na Bahi. Mnamo Machi 2012 ilianzishwa wilaya mpya ya Chemba. Pia Wilaya ya Kondoa imegawiwa sehemu mbili.
Remove ads
Mawasiliano
Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Daressalaam, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kazkazini (Arusha - Kondoa ) kwenda kusini ni nzuri kwa kiwango cha lami. Kuna pia njia ya Reli ya Kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma mjini kuna uwanja wa kitaifa wa ndege.
Remove ads
Hali ya hewa na kilimo
Kwa jumla Dodoma haina mvua nyingi isipokuwa sehemu za wilaya za Mpwapwa na Kondoa. Hivyo hasa mazao yasiyotegemea sana mvua hulimwa kama vile mtama, wimbi, muhogo; kilimo cha mahindi hupatikana mara kwa mara na matatizo ya kukosa mvua. Mazao ya sokoni ni karanga alizeti na simsim. Dodoma ni pia mwanzo wa ustawishaji wa mizabibu na uzalishaji wa divai katika Tanzania.
Kutokana na hali ya hewa mifugo ni mingi (ng'ombe 1,600,000, mbuzi 954,000, kondoo 274,000, nguruwe 23,000, kuku takriban 1,400,000). Idadi ya mifugo imeongeza tatizo la mmomonyoko wa ardhi katika sehemu za mkoa.
Remove ads
Wakazi na utamaduni
Idadi kubwa ya wakazi asilia ni Wagogo.
Kongwa kuna Wakaguru, Wagogo, na Wamasai; na Mpwapwa kuna Wahehe, Wagogo, na Wakaguru.
Kondoa kuna Warangi na pia Wasandawe wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wakushi, Wabantu na Waniloti. Kondoa kuna pia sehemu yenye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale huko Zimbabwe au Afrika Kusini.
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Bahi : mbunge ni Omar Ahmed Badwel (CCM)
- Chemba : mbunge ni Juma Nkamia (CCM)
- Chamwino : mbunge ni Deo Ndejembi (CCM)
- Dodoma Mjini : mbunge ni Antony Peter Mavunde (CCM)
- Kibakwe : mbunge ni George Simbachawene (CCM)
- Kondoa Mjini : mbunge ni Sanda Edwin (CCM)
- Kondoa Vijijini : mbunge ni Dk. Ashatu Kijaji (CCM)
- Kongwa : mbunge ni Job Ndugai (CCM)
- Mpwapwa : mbunge ni George Malima Lubeleje (CCM)
- Mtera : mbunge ni Livingstone Lusinde (CCM)
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads