Wilaya ya Chemba

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wilaya ya Chembamap
Remove ads

Chemba ni jina la wilaya mpya katika mkoa wa Dodoma, Tanzania yenye postikodi namba 41800[1], ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kwa kumega wilaya ya Kondoa[2].

Ukweli wa haraka Nchi, Mikoa ...
Remove ads

Jiografia

Wilaya ya Chemba inapakana na wilaya ya Kondoa upande wa kaskazini, mkoa wa Manyara upande wa mashariki, wilaya ya Chamwino na wilaya ya Bahi upande wa kusini, na mkoa wa Singida upande wa magharibi.

Makao makuu ya wilaya yako Chemba.

Wakazi

Kadiri ya sensa ya mwaka 2012, wilaya ya Chemba ilikuwa na wakazi 235,711.[3] Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 339,333 [4].

Wakazi wengi wa Chemba ni wakulima na wafugaji na mazao yao ni kama vile mahindi, ulezi, alizeti, uwele, udo. Wanyama wanaofugwa ni kama vile ng'ombe, mbuzi, punda na kondoo.

Chemba ni miongoni mwa sehemu ambazo zipo nyuma sana kielimu, pia eneo hili lina shida kubwa ya maji katika vijiji vyake vyote.

Remove ads

Usafiri

Barabara T5 kutoka Dodoma hadi Babati inapitia wilaya hii.[5]

Ugatuzi

Kwa sasa Wilaya ya Chemba inajumuisha tarafa za Goima, Mondo, Kwamtoro na Farkwa pamoja na kata zake 26.[3]

Kata

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads