Machakos

From Wikipedia, the free encyclopedia

Machakos
Remove ads

Machakos ni mji wa Kenya (Ukambani) takriban kilomita 64 upande wa kusini-mashariki wa Nairobi. Ni makao makuu ya kaunti ya Machakos.

Thumb
Machakos, Kenya
Ukweli wa haraka Nchi, Kaunti za Kenya ...

Machakos imekua haraka kwa sababu ni karibu na mji mkuu wa taifa imeshapita idadi ya wakazi lakhi moja na nusu[1]. Wenyeji wa Machakos ni hasa Wakamba.

Remove ads

Historia

Machakos ni kati ya miji ya kwanza ya Kenya bara ikaundwa mwaka 1899 na Waingereza na kuwa makao makuu ya koloni la Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (mbali na eneo lindwa la pwani lililokodishwa na Usultani wa Zanzibar na Uingereza) kwa muda mfupi.

Jina la mji lilitokana na chifu Masaku wa Wakamba aliyewahi kuwa na boma lake hapo.

Baada ya azimio la kutounganisha Machakos na reli ya Uganda mji haukuendelea sana.

Mwaka 2002 majadiliano kati ya pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan yalifanyika Machakos.

Kituo kikuu cha mabasi mjini Nairobi huitwa na wenyeji "Machakos Country Bus".

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads