Manaeni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Manaeni
Remove ads

Manaeni (au Menachem) alikuwa nabii na kiongozi mmojawapo wa Kanisa la kwanza huko Antiokia, jiji la Siria katika Dola la Roma (leo nchini Uturuki).[1]

Thumb
Manaeni akiomba

Katika kutoa taarifa hiyo, Luka mwinjili (Mdo 13:1) anaeleza kwamba alikuwa ndugu wa kunyonya wa Herode Antipa, mtawala wa Galilaya na Perea katika karne ya 1. Hiyo iliweza kumaanisha udugu wa kambo[2] au urafiki wa kudumu tu.

Mwaka 39 Herode Antipa alisafiri kwenda Roma ili kujipendekeza kwa Kaisari Kaligula, kumbe alilazimishwa kubaki ugenini moja kwa moja (Yosefu Flavius, "Ant.", XVIII, vii, 2).

Wakati huohuo Kanisa la Antiokia lilianzishwa na Wakristo wenye asili ya Kiyahudi lakini wa lugha ya Kigiriki, waliotawanyika baada ya dhuluma iliyoanza kwa kifodini cha Stefano mjini Yerusalemu (Mdo 11:19-24). Inafikiriwa kwamba Manaeni alikuwa mmojawao.

Inawezekana alikuwa pia kati ya mashahidi waliompa Luka taarifa mbalimbali, hasa juu ya huyo Herode na ikulu yake (taz. Lk 1:2), na juu ya mwanzo wa Kanisa la Antiokia.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[3].

Sikukuu yake huadhimishwa na Waorthodoksi tarehe 23 Mei[4] lakini na Wakatoliki tarehe 24 Mei[5]

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads