Iringa (mji)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Iringa ni mji mkubwa mojawapo kusini mwa Tanzania wenye hadhi ya manisipaa. Ndiyo makao makuu ya Mkoa wa Iringa na eneo lake linaunda wilaya ya Iringa mjini.

Idadi ya wakazi ni 202,490 (sensa ya mwaka 2022 [1]).


Jina la Iringa lilimaanisha "mahali palipozungukwa na ukuta" kwa maana ya boma. Iringa ya kwanza ilikuwa Kalenga ya leo ambayo wakati wa vita ya Wajerumani dhidi ya Wahehe ilipanuliwa na kuimarishwa na Mtemi Mkwawa wa Wahehe kuanzia mwaka 1887 na kubomolewa na Wajerumani tarehe 31 Oktoba 1894. Mji mpya ulianzishwa na Wajerumani mwaka 1892 kama kituo cha kijeshi juu ya mlima unaotazama mto Ruaha bondeni.
Mji uko kando ya barabara kuu ya TANZAM; kuna usafiri wa kila siku kwenda Dar es Salaam na Mbeya. Njia kwenda Dodoma ni sehemu ya barabara ya kale ya "Cape-Cairo" kati ya Rasi ya Afrika Kusini na Kairo wa Misri na katika miaka ya 2010 imetiwa lami.
Kuna viwanda mbalimbali, hospitali, chuo kikuu na ofisi kuu za dayosisi za Kanisa Katoliki, Walutheri (KKKT) na Waanglikana.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads