Mapinduzi ya utamaduni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mapinduzi ya utamaduni
Remove ads

Mapinduzi ya utamaduni ni mageuzi ya haraka katika siasa na jamii nchini China yaliyotokea katika miaka 1966 - 1976 chini ya uongozi wa Mao Zedong, mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha China.

Thumb
Nyuso za sanamu za zamani za Buddha ziliharibiwa wakati wa mapinduzi hayo. Propaganda ilikuwa inasema: "Bomoa ulimwengu wa kale; tengeneza ule mpya" ikimuonesha Mwanamgambo Mwekundu anayevunja kwa nyundo yake msalaba, Buddha na maandishi ya zamani ya Kichina.

Lengo lilikuwa kusafisha ukomunisti kutoka mabaki yoyote ya utamaduni asili wa nchi hiyo pamoja na ubepari, lakini pia kuimarisha uongozi wa Mao katika chama.

Matokeo yalikuwa aina ya ibada kwa Mao, makumbusho mengi kubomolewa, dhuluma za kila namna dhidi ya mamilioni ya wananchi, watu kuhamishwa kwa lazima, nchi kupooza kisiasa pamoja na kuiathiri kiuchumi.[1]

Mapinduzi hayo yaliathiri Ulaya pia na kuchangia fujo za vijana mwaka 1968 n.k.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads