Maruta
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Maruta (karne ya 4 – 415) alikuwa mmonaki wa Kanisa la Mashariki[1] maarufu kama askofu wa Mayferkat (leo Silvan nchini Uturuki) kwa zaidi ya miaka 10 ambapo alifaulu kuzuia dhuluma ya Dola la Persia dhidi ya Wakristo[2].

Hivyo aliweza kujenga upya makanisa, kukusanya humo masalia ya wafiadini, kuendesha sinodi mbili zilizolipa Kanisa hilo muundo imara, pamoja na kuandika vitabu vya historia ya Kanisa na ufafanuzi wa Biblia, tenzi, anafora n.k.[3]
Rafiki wa Yohane Krisostomo, alishiriki Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (481)[4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Februari[5].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads