Mbamba Bay
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mbamba Bay ni kata na makao makuu ya Wilaya ya Nyasa katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania.
Jina
Maana ya Mbamba Bay ni neno Mbamba ambalo ni jina la mlima uliopo eneo la Zambia na Bay, kama inavyojulikana, ni eneo la bahari lililoingia ndani kama Oyster Bay, Mnazi Bay n.k.
Wakazi
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 13,463 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012, kata ya Mbamba Bay ilikuwa na wakazi wapatao 10,066 waishio humo. [2]


Jiografia
Mji wa Mbamba Bay uko kwenye ufuko wa Ziwa Nyasa takriban km 20 upande wa kaskazini wa mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji.
Usafiri
Kuna bandari inayohudumiwa na meli SV Songea. Kwa ratiba isiyofuatwa mara kwa mara kuna mawasiliano pia na Nkhata Bay huko Malawi, ng'ambo ya ziwa, halafu kwa bandari nyingine za mwambao wa Kitanzania za Ziwa Nyasa hadi Itungi Port.
Kulikuwa na majadiliano ya kujenga reli Mbamba Bay - Mtwara kwa ajili ya usafiri mfupi kati ya Malawi na Bahari Hindi na pia kwa kuboresha maendeleo kusini mwa Tanzania (Mtwara Development Corridor).
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads