Me Against the World
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Me Against the World ni albamu ya tatu ya msanii wa muziki wa hip hop wa Kimarekani, 2Pac. Albamu ilitolewa tarehe 14 Machi 1995 kwenye studio ya Interscope Records.
Albamu ilirekodiwa katika majuma kadhaa kabla msanii hajaendala jela kwa kosa la kumtukana mtu matusi ya nguoni - wakati wa kesi hiyo mnamo mwaka wa 1993 ambayo kulikuwa na mwanamke mmoja wengine wawili ambao wanadai walidhalilishwa na huyu bwana. Ilikuwa hii iliopelekea kifungo cha jela na wengi wanaamini kwamba hii ndiyo iliomwinua kisanaa 2Pac kwenye rekodi, na maujanja yake inaaminika kuwa na alama zaidi za "kukiri," "kutafakari," na "majadilliano-enye moyo safi."[1]
Me Against the World, ilitolewa wakati Tupac yupo jela, ikafanya mgongano wa haraka kwenye chati, ikapanda mpaka nafasi ya kwanza mara tu baada ya kutolewa kwake, na kumfanya 2Pac kuwa msanii wa kwanza kuingiza albamu nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza kwenye chati za Billboard 200 wakati anatumikia kifungo chake jela. Albamu pia ilikuwa ni moja kati ya albamu za 2Pac ambazo zimepokea tathmini nzuri na kuwa na mashabiki wengi na umaarufu kwa ujumla, yenye wengi huiita juhudi yake bora ya kazi yake, na moja kati ya albamu kali za hip hop za muda wote.
Remove ads
Historia
Mwaka wa 1993, Tupac Shakur tayari alishakuwa na mafanikio katika tasnia ya muziki wa hip hop, akiwa na sifa au hati za uthibitisho mbili za dhahabu kwa ajili ya single zake zilizompeleka katika ishirini bora kwa chati za pop ("I Get Around", "Keep Ya Head Up"), na mauzo ya platinum kwa albamu mbili ambazo zimeweza kushika ishirini-na-tano bora za Billboard 200 (Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z.).[2][3] Hata hivyo, msanii huyu mwenye umri wa miaka 22 amepata kuwa na mfululizo wa matukio na kushtakiwa kwa makosa kadha wa kadha ya uvunjaji wa sheria.
Wakati wa kiangazi cha mwaka wa 1993, Shakur alishtakiwa kwa kosa la kumshambulia mwongozaji Allen Hughes wakati wanapiga filamu ya Menace II Society; Shakur baadaye akahukumiwa kifungo cha siku 15 jela. Baadaye, mnamo mwezi wa Oktoba 1993, Shakur alishtakiwa kwa kosa la kuwatandika maofisa wawili wa polisi ambao walikuwa hawapo-kazini huko mjini Atlanta, kulingana na jinsi mashtaka yaliyo hatimaye kesi ikafutwa.
Mnamo mwezi wa Novemba, Shakur na wenzake wawili wa katika msafara wake walishtakiwa kwa kosa la ubakaji wa mshabiki wao wa kike, tukio ambalo walikutwa na makosa na hatimaye kutumikia kifungo cha miaka 4.5 jela.[4] Kulingana na maelezo ya Shakur, albamu ilitengenezwa kwa ajili ya kuonesha wapenzi wa hip hop heshima zake katika sanaa hiyo. Kimashairi, Shakur kimakusudi alijaribu kutengeneza hii kibinafsi zaidi, makini, na juhudi kupita albamu zile za awali.[5]
Remove ads
Orodha ya nyimbo
Remove ads
Historia ya chati
Albamu
Single
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads