Dear Mama
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
"Dear Mama" ni wimbo wa rap ulioimbwa na msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani, 2Pac. Wimbo ulitayarishwa na Tony Pizarro kwa ajili ya albamu ya tatu ya 2Pac Me Against the World, iliyotolewa mnamo 1995. "Dear Mama" ulitungwa na 2Pac kwa ajili ya mama'ke mwenyewe, Afeni Shakur.
"Dear Mama" ulitolewa mnamo tar. 21 Februari 1995 ukiwa kama single ya kwanza kutoka katika albamu. Single hii ilikuwa moja kati ya single zilizopata mafanikio makubwa sana kupita zote zilizotoka kwenye albamu ya Me Against the World. Wimb huu huhesabiwa na watahakiki, mashabiki, na wenye kusisitiza usafaha ikiwa kama moja kati vibao vikali vya hip hop vya muda wote, na kimsingi ni miongoni mwa nyimbo bab-kubwa za 2Pac, kwa kupewa nafasi ya nne kwenye orodha Nyimbo Bora 100 za Rap za About.com.[1]
Remove ads
Uhakiki na mafanikio kibiashara
Wimbo ulichukua nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot Rap Singles kwa takriban majuma matano, kwenye R&B/Hip-Hop Singles ulikaa kwa juma moja, na kushika nafasi ya #9 kwenye chati za Hot 100. Pia ilikaa nafasi ya juu kwenye chati za mauzo ya Hot Dance Music Maxi-Singles kwa takriban majuma manne. Single hii ilitunukiwa Platinum na RIAA mnamo tar. 13 Julai 1995.[2]
Huhesabiwa na wengi kuwa ni kibao cha huzuni zaidi cha 2Pac pia wimbo wenye kuheshiwa sana, na umepata kusifiwa na wasanii wengi tu (Eminem ametaja kama ni wimbo wake kipenzi)[3], tena hata na wasanii wengi ambao hawajihusishi na masuala ya hip hop nao wameusifu. Mnamo 1998, wimbo umeonekana kwenye albamu vya Vibao Vikali vya Tupac. Toleo la pili la wimbo huu ulitayarishwa na Nitty akishirikiana na Anthony Hamilton kwenye toleo la albamu ya Tupac ya 2006, Pac's Life.
Snoop Dogg alisema kwenye mahojiano kwamba kibao hiki kimeonesha upande kamili wa hisia za 2Pac, ambapo imemfanya kuwa tofauti na marapa wengine, kwa sababu "amezama ndani sana", kitu ambacho marapa wengine huwa wanasita au hawana uwezo wa kufanya hivyo.
Wimbo umeonekana kwenye Mfululizo wa FOX New York Undercover.
Remove ads
Muziki wa video
Muziki wa video wa "Dear Mama" uliongozwa na Calvin Caday wakati 2Pac kafungwa; hivyo basi, ameonekana kuwa na mazoea ya wakati wa kama huo kwenye video kwa Tupac. Afeni Shakur pia alishirikishwa, ameonekana kupitia kurasa zilizorushwa za albamu ya picha iliokuwa ikizunguka na kumwonesha picha ya Tupac wakati yungali bwana mdogo. Video pia imeonesha makala fupi inayohusiana na Black Panthers, inadokezea historia yake ya awali kwamba alikuwa mwanachama wa jumuia ya kisiasa.
Remove ads
Orodha ya nyimbo
- 12", Cassette, CD, Maxi[4]
- "Dear Mama" (LP Version) — 4:41
- "Dear Mama" (Instrumental) — 5:21
- "Bury Me a G" — 4:59
- "Dear Mama" (Moe Z. Mix) — 5:09
- "Dear Mama" (Instrumental Moe Z. Mix) — 5:09
- "Old School" (LP Version) — 4:59
Chati zake
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads