Wakopti

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wakopti
Remove ads

Wakopti (au Wakhufti) ni Wakristo asili wa Misri, ambao wanafuata madhehebu ya pekee katika kundi la Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki na wanaunda kundi kubwa zaidi la wakazi wasio Waislamu katika nchi hiyo[1][2][3][4][5][6] .

Thumb
Msalaba wa Kikopti wenye maandishi asili yanayosema: 'Yesu Kristo, Mwana wa Mungu'.
Thumb
Picha ya Kikopti ya Mwinjili Marko, anayehesabiwa kuwa mwanzilishi wa Kanisa la Misri.
Thumb
Rais Nasser wa Misri akipokea ujumbe wa Maaskofu wa Kikopti (1965).
Thumb
Kanisa la Mt. Marko huko Bellaire, Texas, Marekani. Wakopti milioni 4 wanaishi nje ya Misri.

Patriarki wao ni Papa Tawadros II, akiwa na makao makuu jijini Cairo.

Remove ads

Historia

Aina hiyo ya Ukristo ilikuwa anaongoza kabisa kati ya dini za Misri kuanzia karne ya 4 hadi karne ya 6 B.K., lakini baada ya uvamizi wa Waarabu (641), Uislamu ulizidi kuenea kwa njia mbalimbali[7].

Hata hivyo, Wakopti wanabaki asilimia 10-20 ya Wamisri wote[8], isipokuwa wanazungumza Kiarabu, si Kikopti tena, ambacho kinatumika tu katika liturujia.

Wakopti wengine wana ushirika kamili na Kanisa Katoliki, na wengine tena ni Waprotestanti.

Jina Kopti linatokana na Kigiriki Αἰγύπτιος, "Egyuptios", yaani "Mmisri".

Kati ya watakatifu muhimu zaidi wa Kikopti kuna mmonaki Antoni Abati na maaskofu Atanasi wa Aleksandria na Sirili wa Aleksandria.

Mchango mkubwa zaidi walioutoa ni kuanzisha umonaki na kutetea umungu wa Yesu Kristo pamoja na usahihi wa kumuita Bikira Maria "Mama wa Mungu".

Kutoka Misri, Ukristo wa aina hiyo ulienea tangu zamani hasa Sudan, Ethiopia na Eritrea.

Siku hizi Wakopti wengi wanazidi kuhamia nchi nyingine, hasa za Magharibi[9].

Jumla yao imekadiriwa kuwa milioni 18-22.[10][11][12]

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads