Monrovia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Monrovia ni mji mkuu wa Liberia. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2008, mji huu ulikuwa na wakazi wapatao 1,021,762.


Historia
Eneo uliko mji huo mwanzoni liliitwa na mabaharia Wareno Cape Mesurado walipowasilia katika miaka ya 1560. Wakati huo tayari kulikuwa na wakazi wakiishi hapo.
Mji ulianza kujengwa mwaka 1822 na chama cha American Colonization Society ikiwa ni makazi ya watu waliokombolewa toka utumwani nchini Marekani.[1] Jina Monrovia lilitokana na jina la Rais wa Marekani James Monroe.
Watu wa kwanza kuhamia Monrovia toka nchini Marekani waliwasili mwaka 1822 katika Kisiwa cha Sherboro nchini Sierra Leone. Wahamiaji wengi walifariki baada ya kuwasili Monrovia.
Mkutano wa kutunga katiba ya Liberia wa American Colonization Society ulifanyikia Monrovia mwaka 1845.
Remove ads
Uchumi
Uchumi wa Monrovia unategemea zaidi bandari yake na madini ya chuma. Bidhaa kama vile saruji, mafuta, matofali, vigae, samani, na kemikali zinatengenezwa Monrovia.
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads