Umba (mto)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Umba (mto)
Remove ads

Umba ni mto wa Tanzania kaskazini mashariki unaopita katika Mkoa wa Tanga na kuishia nchini Kenya.

Thumb
Ramani ya mto Umba.

Chanzo chake kipo katika milima ya Usambara katika msitu wa Shagayu kwa kimo cha mita 2,000 juu ya UB.

Unapita Mlalo na kuendelea kutelemka haraka kuelekea pwani ikipokea mito ya kando kutoka milima ya Usambara[1].

Kilomita chache kabla ya kufika Bahari ya Hindi inavuka mpaka wa Kenya (kaunti ya Kwale).

Mdomo wa Umba kwenye bahari hiyo ulipangwa mwaka 1890 baina ya Ujerumani na Uingereza kuwa mpaka wao. Hadi leo sehemu hii ni chanzo cha mstari wa mpaka kati ya Tanzania na Kenya unaoendelea bila kunyoka hadi Ziwa Jipe, ukifuata mitelemko ya mlima Kilimanjaro na kuendelea hadi Ziwa Viktoria.

Tangu miaka ya 1960 vito mbalimbali vimepatikana katika maeneo ya juu ya Umba.[2] Kuna hifadhi ya wanyamapori ya mto Umba, pamoja na hifadhi ya Mkomazi, jumla kilomita za mraba 2,600.

Beseni la mto Umba huwa na km² 8,070 na kati ya hizo km² 2,560 ziko upande wa Kenya. Matawimto mengi yanaingia kutoka kusini, chache kutoka kaskazini. Beseni la Umba hupokea takriban milimita 600 za mvua kwa mwaka.[3]

Remove ads

Hidrometria

Kiasi cha maji kinachopita katika Umba kimepimwa kwenye kituo cha Mbuta takriban km 40 kabla ya mdomo wake. Hapo chini ni wastani ya kiasi cha maji kwa /s kwenye kituo cha Mbuta kwa kipindi cha miaka 30 ya 19541984)[4]

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads