Nandy
Muimbaji kutoka nchini Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nandy (amezaliwa Kilimanjaro, Tanzania, 9 Novemba, 1992) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania.
Mnamo mwaka 2017 alishinda tuzo ya All Africa Music Awards katika kundi la wasanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki.[1][2]
Remove ads
Maisha ya awali
Nandy alizaliwa na Mary Charles, fundi kushona, na Charles Mfinanga, ambaye ni fundi makenika. Jina la Nandy ni kifupi cha jina lake halisi Nandera. Alianza kutumbuiza akiwa na umri mdogo kabisa. Akiwa na miaka mitano, alikuwa mwanachama hai wa kwaya ya mafunzo ya Jumapili ya Kanisa la KKKT huko Moshi. Alimaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Mawenzi, baadaye alijiunga Lomwe High School ambako huko alikuwa mwana-kwaya mkuu katika shule hiyo. Baada ya kumaliza elimu ya juu alijiunga na Chuo cha Biashara (CBE), Dar es Salaam, Tanzania.
Remove ads
Kazi
Tanzania House of Talent
Kazi yake ilianza kujulikana baada ya rafiki yake kumtambulisha kwa Ruge Mutahaba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania House of Talent (THT). Hapa ndipo alipokutana na Ema the Boy, ambaye ndiye aliyekuja kumtayarishia kibao chake maarufu cha Nagusagusa.Wimbo ulikuja kutamba mno wiki tu tangu kutolewa kwake.
Mwanzoni mwa mwaka wa 2016 alishiriki kwenye mashindano ya kuimba yaliyoandaliwa na Tecno. Shindano lilishirikisha washiriki wengine kutoka nchi kibao za Afrika na kipindi cha fainali kilichofanyika huko Lagos, Nigeria, Nandy aliibuka kama mshindi wa pili. Shindano hili lilimkuza kimuziki, hasa katika suala zima la utumbuizaji jukwaani, alipata maarifa ya muhimu kutoka kwa magwiji wa muziki kama vile akina M.I Abaga, Yemi Alade na Bien wa Sauti Sol.[3][4]
Mwaka 2017 alitoa kibao cha One Day ambacho kilisukuma kazi yake na hatimaye kumpa nafasi kadhaa zilizomfanya kushiriki kwenye Coke Studio Africa 2017 na mwaka huohuo akaja kuchaguliwa kwenye tuzo za All Africa Music Awards katika kundi la wanamuziki bora wa kike kutoka Afrika Mashariki na kuibuka mshindi na akatoa kibao kiitwacho kivuruge na hivi sasa anatamba na wimbo wake ambao amefanyakazi yeye na willy paul ambao jina lake ni hallelujjah[5][6][7][8][9]
Mbali na muziki, yeye ni mpenda mitindo na ndiye mmiliki wa Prints by Nandy Africa. Yeye pia ni balozi wa UNICEF, mwanamitindo wa nguo za harusi za kina dada na miliki wa Make up by Nandy.[10]
Albamu
- African Princess (2018)[11]
Singo
Remove ads
Tuzo na chaguzi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads