Ndezi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ndezi ni wagugunaji wakubwa wa familia Thryonomyidae ambao wana mnasaba karibu kiasi na nungunungu. Wanatokea mahali panyevu pa Afrika kusini kwa Sahara. Wamo miongoni mwa wagugunaji kubwa kabisa duniani. Mwili wao una urefu wa sm 35-60 na uzito wa kg 6-10. Wana manyoya magumu yenye rangi ya kahawa na vidoa kijivu na njano. Hula manyasi ya maji porini lakini katika maeneo ya kilimo hula mimea ya shamba kama muwa, muhogo n.k. Wanaweza kudidimiza hasara kubwa. Ndezi hufugwa sana huko Benini na Togo, na hata nchini Kameruni, Kodivaa, Gaboni, Gana, Nijeria, Senegali na Kongo wakulima wahimizwa kufuga wanyama hawa. Nyama yao ni nzuri sana..
Remove ads
Spishi
- Thryonomys gregorianus, Ndezi Mdogo (Lesser Cane Rat)
- Thryonomys swinderianus, Ndezi Mkubwa (Greater Cane Rat)
Picha
- Ndezi waliogwiwa nchini Kodivaa
- Ndezi afugwaye nchini Gaboni
- Ndezi afugwaye nchini Kameruni
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads