Gabon
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Gabon, rasmi Jamhuri ya Gabon (Kifaransa: République gabonaise), ni nchi iliyo kwenye pwani ya Atlantiki ya Afrika ya Kati, kwenye ikweta, iliyopakana na Guinea ya Ikweta kaskazini-magharibi, Kamerun kaskazini, kusini Jamhuri ya Kongo, na Jamhuri ya Guinea-magharibi. Ina eneo la kilomita za mraba 270,000 (100,000 sq mi) na idadi ya watu milioni 2.3. Libreville ndio mji mkuu wa nchi na jiji kubwa zaidi.
Nchi hii ina umma mdogo, madini na mali kwa wingi, na wafanyabiashara kutoka nchi za kigeni wameweza kufanya Gabon iwe nchi yenye maendeleo makubwa.
Remove ads
Jiografia
Maeneo ya utawala
Gabon imegawiwa katika mikoa 9 nayo ina jumla ya wilaya (départements) 37.
Mikoa ni:
Historia

Jamhuri ya Gabon, tangu kupata uhuru kutoka Ufaransa tarehe 17 Agosti 1960, imeongozwa na Rais watatu, Léon M'ba, El Hadj Omar Bongo ambaye amekuwa kiongozi kutoka mwaka wa 1967 hadi kifo chake (2009: ndiye aliyekuwa kiongozi barani Afrika aliyeshikilia uongozi kwa muda mrefu zaidi), halafu mwanae Ali aliyepinduliwa na wanajeshi tarehe 30 Agosti 2023.
Remove ads
Siasa

Mwaka wa 1990 Gabon ilianza demokrasia ya vyama vingi na katiba ya kidemokrasia ili ruhusu ukweli wa uchaguzi na uwajibikaji wa idara za serikali, lakini hali iliendelea kuwa karibu ileile.
Uchumi
Gabon ni nchi yenye neema sana kuliko nchi jirani. Uchumi wake, hasa chumo cha umma, ni mara nne ya nchi za Afrika kusini kwa Sahara. Hii hasa ni kwa sababu ya uzalishaji wa mafuta ambao umeleta utajiri na mali, lakini usambazaji wa mali hii ya mafuta bado umedhoofika.
Gabon ilikuwa mwanachama wa Muungano wa Nchi Zinazouza Mafuta (OPEC) kutoka mwaka wa 1975 mbaka 1995.
Mwaka 1990, udhaifu wa pesa CFA frank uliacha Gabon katika shida ya kulipa deni za kimataifa; Ufaransa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wameipa Gabon mkopo na usaidizi kwa uelewano kwamba Gabon itageuza uchumi wake barabara.
Remove ads
Watu
Yasemekana mambo ya mazingira yalifanya umma wa Gabon kutopanda kwa sensa kati ya miaka 1900 na 1940.
Ni nchi ambayo ina umma mdogo zaidi katika Afrika bara, na upungufu wa wafanyakazi ni mojawapo ya mambo yanayofanya hasa uchumi kutovuma zaidi.
Umma hasa kwa ujumla ni kama watu milioni 2.4.
Gabon hasa ina makabila zaidi ya 40 ambayo yana utamaduni na lugha tofauti lakini karibu wote (95%) ni wa jamii ya Bantu. Wafang ndio kabila kubwa zaidi nchini Gabon, wengine ni Wamyene, Wabandjabi, Waeshira, Wabapounou na Waokande.
Lugha ya Kifaransa ndiyo lugha rasmi ya taifa ambayo hutumika kwa mawasiliano (wakazi wanaoimudu ni 80%). Wafaransa 10,000 wanaishi Gabon, na Ufaransa unaathiri mambo ya kigeni, utamaduni na biashara nchini Gabon.
Upande wa dini, imekadiriwa kwamba 75.6% za wakazi ni Wakristo (hasa Wakatoliki), 12.2% ni Waislamu (hasa wageni), na 5.7% wanafuata dini asilia za Kiafrika (Bwiti).
Remove ads
Utamaduni
- Makabila ya Gabon
- Muziki wa Gabon
- Orodha ya lugha za Gabon
Tazama pia
- Mawasiliano nchini Gabon
- Mambo ya kigeni ya Gabon
- Orodha ya kampuni za Gabon
- Jeshi la Gabon
- Historia ya Gabon
- Uchukuzi nchini Gabon
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Marejeo
- David E. Gardinier, Kamusi ya Historia ya Gabon, tolezi ya 2. (The Scarecrow Press, Inc., 1994) – kazi inayohusu maelezo biografia ya vifaa 1,453
- James F. Barnes, Gabon: Beyond the Colonial Legacy (Boulder: Westview, 1992)
Viungo vya nje
Serikali
- Le Gabon : makala rasmi ya Jamhuri ya Gabon Ilihifadhiwa 29 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Assemblée nationale du Gabon makala rasmi.
- Gabonese Embassy in London Ilihifadhiwa 22 Septemba 2019 kwenye Wayback Machine. arithio za serikali
- Le Sénat de la République Gabonaise makala rasmi (kwa kifaransa)
Habari
- AllAfrica.com - Gabon viungo via taarifa ya habari
Uchambuzi
Koo na makabila
- Baka watu wafupi wa Kamerun na Gabon Utamaduni na wakazi wa kwanza Gabon
Maelekezo
- Open Directory Project - Gabon Ilihifadhiwa 24 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine. maelekezo
- Chuo kikuu cha Stanford – Afrika kusini mwa sahara: Gabon maelekezo
- Chuo kikuu cha Pennsylvania – Ustadi wa-Afrika: Gabon maelekezo
- Yahoo! - Gabon Ilihifadhiwa 28 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine. directory category
Utalii
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Gabon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads