Ndui

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ndui
Remove ads

Ndui (kwa Kiingereza: smallpox) ilikuwa ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na aina mbili za virusi: Variola major na Variola minor.

Thumb
Mtoto wa Bangladesh aliyepatwa na ndui mwaka 1973.

Ulikuwa unaleta kifo cha waliopatwa kwa asilimia 30-35, lakini zaidi kati ya watoto.

Walionusurika wengi waliachwa na makovu ya kudumu hasa katika uso.

Historia

Inakadiriwa ulikuwepo tangu miaka ya 10000 KK hadi mwaka 1977.

Chanzo chake hakijulikani lakini kuna dalili ya kwamba ilitokea mapema sana katika Misri ya Kale[1]. Pengine farao Ramses V alikuwa mgonjwa wa kwanza anayejulikana kutokana na utafiti wa mumia yake[2].

Labda ilipelekwa Uhindi na wafanyabiashara Wamisri mnamo miaka ya 1500 KK. Ugonjwa uliua watu wengi huko Ulaya[3], Asia na Afrika ilikosambaa pia.

Matokeo ya ndui yalikuwa mabaya hasa Amerika ambako Waindio yaani wakazi asilia waliwahi kuishi milenia nyingi bila mawasiliano na bila maambukizi kutoka sehemu nyingine za dunia, hivyo walikosa kabisa kinga. Kwa mfano Wahispania waliweza kuvamia milki ya Azteki huko Mexiko kwa sababu wateteaji wa Tenochtitlan walidhoofishwa na ugonjwa uliopelekwa hapo na Wahispania.

Mwaka 1967 tu ndui iliua watu milioni mbili na katika karne ya 20 kwa jumla milioni 300 au 500.

Remove ads

Chanjo

Thumb
Tangazo la kuhamasisha watu kushiriki katika chanjo ya ndui.

Nchini China na Uhindi ilijulikana tangu kale kwamba kumdunga mtu kwa majimaji kutoka vidonda vya ndui kunasababisha homa kidogo lakini kunamkinga dhidi ya maambukizi makali[4] hata kama takriban asilimia 1-2 ya watu waliodungwa vile walikufa[5].

Mnamo 1796 tabibu Mwingereza Edward Jenner alitambua kwamba kumdunga mtu kwa majimaji ya vidonda vya ndui ya ng'ombe kunamkinga pia dhidi ya ndui wa kibinadamu, lakini bila matatizo yale yaliyoweza kutokea kwenye mbinu ya awali. [6] Chanjo hiyo iliboreshwa na kupunguza kutokea kwa ndui, Nchi nyingi duniani ziliweka taratibu za kutoa chanjo kwa watoto wote. Tangu mwaka 1967 Shirika la Afya Duniani WHO lilianzisha mradi wa kutafuta wagonjwa wa mwisho wa ndui na kuwatibu. Mgonjwa wa mwisho alipatikana nchini Somalia kwenye mwaka 1976[7].

Tangu siku zile ndui ni ugonjwa wa kwanza ambao binadamu kwa njia ya chanjo alifaulu kuukomesha.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads