Bangladesh
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bangladesh (pia: Bangladesh; kwa Kibengali: বাংলাদেশ, bāṃlādeś) ni nchi ya Asia ya Kusini. Imepakana na Uhindi pande zote barani isipokuwa mpaka mfupi wa km 193 na Myanmar upande wa kusini-mashariki na pwani ya Ghuba ya Bengali.Ni nchi ya nane kwa kuwa na watu wengi zaidi duniani na miongoni mwa nchi zenye msongamano mkubwa wa watu na wakazi wanaozidi milioni 170 ndani ya eneo la kilomita za mraba 148,460.Dhaka ndio mji mkuu na jiji kubwa zaidi, ni kituo cha kitaifa cha kisiasa, kifedha na kitamaduni
Remove ads
Jiografia
Sehemu kubwa ya nchi ni delta ya mito Ganga na Brahmaputra.
Uso wa nchi ni tambarare na mita chache tu juu ya uwiano wa bahari. Hivyo wananchi huteswa mara nyingi na mafuriko makali.
Historia
Bangladesh ni sehemu ya mashariki ya Bengali ya kihistoria ambayo ilikuwa ndani ya Uhindi wa Kiingereza hadi 1947.
Mwaka 1857 Wahindi walipinga utawala wa Kampuni ya Kiingereza kwa Uhindi wa Mashariki. Matokeo yake utawala ulishikwa na serikali yenyewe ya Uingereza kama koloni (1858).
Mwisho wa karne ya 19 harakati za Wahindi kutafuta uhuru zilianza upya. Mwaka 1885 chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa na Wahindu na Waislamu pamoja waliodai uhuru.
Mwaka 1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "Shirikisho la Waislamu".
Mwaka 1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili.
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.
Tarehe 14/15 Agosti 1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili za Uhindi na Pakistan. Mgawanyo wa Uhindi ulikuja na vita na kumwaga kwa damu nyingi. Bengali yenyewe iligawanyika kwa sababu wakazi wengi wa mashariki walikuwa Waislamu, tofauti na Wabengali wengine waliokuwa Wahindu.
Tarehe 30 Januari 1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka usawa wa Waislamu na Wahindu.
Wakati ule Bengali ya mashariki ilikuwa nchi moja pamoja na Pakistan ya leo, bila kujali umbali mkubwa kati ya pande hizo mbili zilizounganishwa na dini.
Iliitwa "Pakistan ya Mashariki" mpaka mwaka 1971 ilipojitenga na Pakistan kwa msaada wa India katika Vita vya Uhuru vya Bangladesh.
Remove ads
Watu
Kati ya nchi kubwa, Bangladesh inaongoza kwa msongamano wa watu. Uzazi umepunguzwa sana na kampeni za udhibiti wake zilizofanywa miaka ya mwisho.
Wabengali ni asilimia 98 za wakazi, lakini kuna pia makabila madogo 11.
Asilimia hizohizo wanaongea Kibengali, ambacho ndicho lugha rasmi. Kiingereza pia kinatumika sana.
Upande wa dini, Waislamu ni asilimia 86-90 (wengi wakiwa Wasuni), Wahindu ni asilimia 8-12, Wabuddha ni asilimia 0.6 na Wakristo (hasa Wakatoliki, halafu Waprotestanti) asilimia 0.4.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads