Nemesiani na wenzake
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nemesiani na wenzake Feliche, Lucho, Feliche, Liteo, Poliano, Vikta, Iader na Dativus (walifariki 258 hivi) walikuwa maaskofu ambao, pamoja na mapadri, mashemasi na waumini wengine wa Numidia (eneo la Algeria ya leo), baada ya kupigwa kikatili walifungwa pingu na kupelekwa Sigum kufanya kazi ya shokoa katika migodi wakifia hivyo dini ya Ukristo chini ya makaisari Valerian na Galienus [1].
Sipriani mfiadini, askofu mkuu wao, aliwaandikia barua ya kuwatia moyo wavumilie kwa imara na kushika amri za Bwana, pamoja na kuwatumia misaada, nao walijibu barua tatu kutoka sehemu tofauti [2].
Tangu kale wanaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 10 Septemba[3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads