Njia ya Msalaba

From Wikipedia, the free encyclopedia

Njia ya Msalaba
Remove ads

Njia ya Msalaba (kwa Kilatini, Via Crucis au Via Dolorosa) ni desturi ya sala inayolenga kumfuata Yesu Kristo hadi msalabani na kaburini.

Thumb
Kituo cha 10 – Yesu akivuliwa. Kanisa kuu la Santiago de Compostela, Hispania.
Thumb
Kituo cha 12 – Yesu akifa msalabani. St. Raphael's Cathedral, Dubuque, Iowa, Marekani.
Thumb
Njia ya msalaba ilivyopangwa katika kanisa kuu la Hong Kong, China.
Thumb
Station 5: Simoni wa Kirene akimsaidia Yesu kubeba msalaba, Maandamano ya Ijumaa Kuu 2011 huko Ulm, Ujerumani.

Desturi hiyo ilianza Wakristo wa Ulaya walipozidi kutembelea Nchi takatifu katika Karne za Kati. Ni hasa wafuasi wa Fransisko wa Asizi walioeneza desturi hiyo kila mahali.[1]

Mengi kati ya makanisa ya Wakatoliki yaani picha 14 zilizopangwa kwa kawaida ukutani kwa umbali fulani ili kuwezesha waamini kutembea kati ya moja na nyingine huku wakiendelea kutafakari juu ya mateso ya Yesu, jinsi ambavyo wangefanya mjini Yerusalemu, ili kuelewa zaidi upendo wa Mungu, kuchukia dhambi na kuzifidia.[2][3]

Hata baadhi ya Walutheri na Waanglikana wanapenda desturi hiyo.[4][5]

Desturi hiyo inaweza kufuatwa na mtu mmojammoja au kwa makundi hata makubwa.[6]

Mbali ya kila Ijumaa ya mwaka, waamini wengi wanafuata njia hiyo wakati wa Kwaresima, na kwa namna ya pekee Ijumaa Kuu.[7]

Mbali ya vituo 14 vilivyozoeleka zaidi, wengine wanapenda kuviongeza, kuvipunguza au kuvibadilisha hasa kwa kufuata zaidi habari za Injili[8][9] na kumalizia na ufufuko wake.[10][11]

Remove ads
Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads