Nzinga Nkuwu
mfalme wa kwanza wa ufalme wa Kongo From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nzinga Nkuwu (baadaye João I kwa Kireno: 1440 hivi - 1509) alikuwa Manikongo wa 5 wa Ufalme wa Kongo kuanzia mwaka 1470 hadi kifo chake. Aliongokea Ukristo akabatizwa tarehe 3 Mei 1491 lakini baadaye alirudia dini ya jadi hasa kwa kushindwa kuacha desturi ya mitara.

Baada yake alitawala kwa miaka mingi mwanae Afonso I aliyejitahidi sana kufanya ufalme wote ufuate imani na maadili ya Kanisa Katoliki kwa msaada wa mtoto wake Henri wa Kongo, askofu wa kwanza kutoka Afrika kusini kwa ikweta.
![]() |
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nzinga Nkuwu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads