Observansya

From Wikipedia, the free encyclopedia

Observansya
Remove ads

Observansya (kwa Kilatini: observantia, kwa Kiingereza: observantism, observant movement au observant reform) ilikuwa tapo la urekebisho lililoenea katika mashirika mbalimbali ya kitawa ya Kanisa la Kilatini kuanzia katikati ya karne ya 14 hadi katikati ya karne ya 16 au Mtaguso wa Trento (15451563).

Thumb
Livio Mehus, Mtakatifu Petro wa Alkantara akimkomunisha mtakatifu Teresa wa Avila; mchoro huu wa mwaka (1683) unaotunzwa Prato (Italia) unaonyesha wawili kati ya viongozi wakuu wa observansya, mmoja mwanamume Mfransisko, wa pili mwanamke Mkarmeli.

Watawa hao walikusudia kushika sawasawa kanuni zao (kwa Kilatini: observantia regulae) kama ilivyokuwa mwanzoni, dhidi ya ulegevu uliosambaa kwa kawaida baada ya kifo cha waanzilishi, na hasa kutokana na tauni iliyoua karibu nusu ya wakazi wote wa Ulaya (1346-1353) ikifuatwa na Farakano la Kanisa la Magharibi (1378-1417).

Juhudi zao zilijitokeza na kukubaliwa na watawa wengi, hazikutokana na maagizo ya Mapapa yaliyolenga kuweka mambo sawa, kama yale ya Papa Benedikto XII miaka 13351339.

Kati ya mashirika yaliyoguswa zaidi na tapo hilo kuna Waaugustino, Wabenedikto, Wakarmeli, Wadominiko na hasa Wafransisko.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads