Off the Wall

From Wikipedia, the free encyclopedia

Off the Wall
Remove ads

Off the Wall ni albamu ya tano ya hayati mwanamuziki wa Kimarekani, Michael Jackson. Albamu ilitolewa mnamo tar. 10 Agosti 1979 kupitia studio ya Epic Records, baada ya Jackson kupata sifa kemkem pale alipoimba katika filamu ya The Wiz. Wakati akiifanyia kazi albamu hii, Jackson na Quincy Jones wakawa marafiki wakubwa, na Jones akakubali kufanya kazi na Jackson katika albamu yake iliyofuata.

Ukweli wa haraka Studio album ya Michael Jackson, Imetolewa ...

Kazi ya kurekodi albamu hii ilichukua nafasi kati ya Desemba 1978 na Juni 1979 katika studio ya Allen Zentz Recording, Westlake Recording Studios, na Cherokee Studios ya mjini Los Angeles, California. Jackson ameshirikiana vilivyo kabisa na watunzi wa nyimbo wengine kama vile Paul McCartney, Stevie Wonder na Rod Temperton. Jackson ameandika nyimbo kadhaa mwenyewe. Nyimbo hizo ni pamoja na single kiongozi kutoka katika albamu hii, "Don't Stop 'til You Get Enough".

Rekodi hii iliamishwa kutoka katika studio ya awali ambayo Jackson alikuwa akifanyanayo kazi, Motown. Kuna maelezo kadhaa yanayotaja kwamba Off the Wall imeimbwa kwa mtililiko wa funk, disco-pop, soul, soft rock, jazz na pop. Jackson amepata pongezi nyingi sana kwa uimbaji wake wa katika albamu hii.

Rekodi imepata pongezi nyingi na imempelekea Michael kushinda tuzo yake ya kwanza ya Grammy Awards tangu miaka ya 1970. Kwa albamu ya Off the Wall, Jackson akawa msanii pekee wa kujitegemea kuwa na single nne zilizoingia katika 10 bora za Billboard Hot 100 kutoka katika albamu moja. Albamu ilipata mafanikio makubwa ya kibiashara, hadi leo hii imetunukiwa platinamu 7 katika Marekani na kuuza nakala milioni 20 dunia kote.

Mnamo tar. 16 Oktoba 2001, toleo maalumu la Off the Wall lilitoloewa tena na studio ya Sony Records. Ripoti ya hivi karibuni ya Allmusic na Blender inaonyesha bado wanaendelea kuisifu Off the Wall kwa kukata rufaa katika karne ya 21. Mnamo mwaka waIn 2003, albamu imeshika nafasi ya 68 katika orodha ya albamu bora 500 za karne iliyochini ya gazeti la Rolling Stone. Katika National Association of Recording Merchandisers wameiorodhesha kwenye namba 80 kutoka katika orodha ya albamu 200 bora za kale. Mnamo mwaka wa 2008, Off the Wall imepata kuwekwa katika Grammy Hall of Fame.

Remove ads

Historia

Mauzo

Maelezo zaidi Nchi, Matunukio ...

Orodha ya nyimbo

Maelezo zaidi #, Jina ...
Maelezo zaidi Toleo Maalumu la 2001, # ...
Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads