Orsisius

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Orsisius (kwa Kimisri: Oresiesis-Heru-sa Ast; alifariki 380) alikuwa Mkristo wa Misri, ambaye alimfuata Pakomi jangwani akamsaidia kutunga kanuni ya kwanza kwa ajili ya jumuia za wamonaki[1].

Kiongozi wa monasteri katika kisiwa cha Tabenna, alipofariki Pakomi (348) alichaguliwa kushika nafasi yake, lakini alimuachia Theodori. Baada ya huyo pia kufariki (380 hivi), ndipo tu alipokubali kwa shauri la Atanasi wa Aleksandria.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Juni.

Remove ads

Maandishi

Jeromu alitafsiri baadhi ya maandishi yake[2]

Vyanzo

  • "Orsisius". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads