Papa Adeodato I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Adeodato I (pia Adeodatus, Deodatus, Deusdedit) alikuwa Papa kuanzia tarehe 19 Oktoba 615 hadi kifo chake tarehe 8 Novemba 618[1]. Alitokea Roma, Italia[2]. Jina la baba yake lilikuwa Stephanus, ambaye alikuwa shemasi mdogo.

Alimfuata Papa Bonifasi IV akafuatwa na Papa Bonifasi V.
Kabla ya kuchaguliwa, alitoa huduma ya kipadri kwa miaka 40[3]. Alikuwa padri wa kwanza kuchaguliwa kuwa Papa tangu Yohane II mwaka 533. Baadaye alikuza idadi ya mapadri na kuwapa nafasi zilizokuwa zimeshikwa na wamonaki kadiri ya sera ya Papa Gregori I na Papa Bonifasi IV[4][3].
Kweli alijulikana kwa kupenda wakleri na waumini wake pamoja na unyofu na hekima yake [5].

Matumizi ya kwanza ya mihuri ya risasi au bullae kwenye nyaraka za Kipapa yanahusishwa naye.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[6].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads