Papa Felix IV

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Felix IV
Remove ads

Papa Felix IV (490 hivi - 20/22 Septemba 530) alikuwa Papa kuanzia tarehe 12 Julai 526 hadi kifo chake[1]. Alitokea Campania, Italia[2]. Baba yake aliitwa Castorius.

Thumb
Mozaiki ya Mt. Felisi IV.

Alimfuata Papa Yohane I akafuatwa na Papa Bonifasi II.

Alichaguliwa kwa kumridhisha mfalme Theodoriko Mkuu akaweza kupata kwake fadhili mbalimbali kwa Kanisa Katoliki[3]. Mfalme alipofariki mwaka uleule, Felix aliweza kuendesha Kanisa kwa uhuru zaidi[4].

Aligeuza mahekalu mawili ya Kipagani ya mjini Roma kuwa basilika la Wat. Kosma na Damiani na alipigania sana imani sahihi[5].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 12 Oktoba[6].

Remove ads

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads