Papa Yohane I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Yohane I alikuwa Papa kuanzia tarehe 13 Agosti 523 hadi kifo chake tarehe 18 Mei 526[1]. Alitokea Toscana, Italia[2].

Alimfuata Papa Hormisdas akafuatwa na Papa Felisi IV.
Alitumwa na mfalme Theodoriko Mkuu kwa Kaisari Yustino I wa Konstantinopoli[3][4] ili Waario wasiendelee kudhulumiwa. Alikuwa Papa wa kwanza kuadhimisha sadaka ya Pasaka katika mji huo. Ingawa alifaulu walau kiasi katika lengo la mfalme, aliporudi Italia alifungwa naye hadi akafa kwa magumu yaliyompata gerezani [5].
Tangu kale ameheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads