Papa Marcellinus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Marselino alikuwa Papa kuanzia tarehe 30 Juni 296 hadi kifo chake tarehe 25 Oktoba 304[1]. Alitokea Roma, Italia[2].

Alimfuata Papa Kayo akafuatwa na Papa Marcellus I.
Tangu mwaka 302, Kanisa liliteseka sana chini ya Kaisari Diokletiano, aliyechochewa na kaisari Galerius. Ilisemekana kwamba Marcellinus pia aliyumba kwa muda mfupi, ila Augustino alikanusha taarifa hiyo[2].
Ikiwa Marcellino aliuawa au kufa kwa uzee, hakuna uhakika[3].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[4].
Sikukuu yake kwa Wakatoliki ni 26 Aprili (ingawa hatajwi tena katika Martyrologium Romanum[5]) ila kwa Waorthodoksi ni tarehe 7 Juni.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads