Papa Marcello I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Marcello I
Remove ads

Papa Marcello I alikuwa Papa kuanzia mwaka 306 hadi kifo chake tarehe 16 Januari 309[1]. Alitokea Roma, Italia.

Thumb
Papa Marcello I.

Alimfuata Papa Marcellinus miaka miwili hivi baada ya huyo kufa wakati wa dhuluma ya Kaisari Diokletiano dhidi ya Wakristo[2] .

Katika kurudisha taratibu za Kanisa, alipanga malipizi makali kwa waumini wengi waliowahi kuasi. Kadiri ya Papa Damaso I, Marseli alikuwa mchungaji bora, aliyepingwa vikali na Wakristo waasi waliokataa kufanya toba aliyokuwa ameiagiza[2], akasingiziwa akafungwa na Kaisari Maxentius na kufariki mapema uhamishoni, akifuatwa madarakani na Papa Eusebius[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 16 Januari[4].

Remove ads

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads