Papa Siricius
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Siricius alikuwa Papa kuanzia tarehe 15 au 22 au 29 Desemba 384 hadi kifo chake tarehe 26 Novemba 399[1]. Alitokea Roma, Italia na baba yake aliiitwa Tiburtius.

Alimfuata Papa Damaso I[2] akafuatwa na Papa Anastasius I.
Alikuwa mtendaji na kukabili masuala mbalimbali. Amri zake 15 (hati Directa) kuhusu maisha ya Kanisa ni za kwanza kutufikia nzima bila kasoro.
Ambrosi alimsifu kama mwalimu halisi kwa sababu, akibeba mzigo wa wale wote wenye majukumu ya kiaskofu, aliwaelimisha kuhusu mafundisho ya mababu wa Kanisa, aliyoyathibitisha kwa mamlaka yake ya Kipapa pia[3].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads