Pat Nixon
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Thelma Catherine "Pat" Nixon (16 Machi 1912 - 22 Juni 1993) alikuwa mke wa Richard Nixon, Raisi wa 37 wa Marekani, na alihudumu kama Mwanamke wa Kwanza wa Marekani kuanzia mwaka wa 1969 hadi 1974.[1]
Alizaliwa Ely, Nevada, alikua pamoja na kaka zake wawili katika eneo linalofahamika kwa sasa kama Cerritos, California, na alihitimu Excelsior Union High School huko Norwalk, California mwaka 1929. Pia alisoma Chuo cha Fullerton Junior na baadaye Chuo Kikuu cha Southern California. Alilipia masomo yake kwa kufanya kazi kadhaa, ikiwa ni pamoja na meneja wa duka la dawa, mwandishi, mpiga picha za mionzi na karani wa rejareja. Mnamo mwaka 1940, aliolewa na mwanasheria Richard Nixon na kupata watoto wawili wa kike, Tricia and Julie.Wanandoa hao waliitwa "Timu ya Nixon", ambapo Richard na Pat Nixon walifanya kampeni pamoja katika uchaguzi wake wa mafanikio wa Bunge la Marekani wa mwaka 1946 na 1948. Richard Nixon alichaguliwa kuwa makamu wa rais mwaka 1952 pamoja na Jenerali Dwight D. Eisenhower, na hapo Pat akawa second lady. Pat Nixon alibadilisha sana nafasi hiyo kwa kusisitiza kutembelea shule, vituo vya kulelea yatima, hospitali, na masoko ya vijijini aliposhiriki katika misheni nyingi za upatanisho duniani kote.
Akiwa first lady, Pat Nixon alihamasisha shughuli nyingi za hisani, ikiwa ni pamoja na kazi za kujitolea. Alisimamia ukusanyaji wa zaidi ya vipande 600 vya sanaa na samani za kihistoria kwa ajili ya White House, mkusanyiko mkubwa zaidi kuliko utawala wowote uliopita. Alikuwa first lady aliyezuru nchi nyingi zaidi katika historia ya Marekani, rekodi ambayo haikuvunjwa hadi miaka 25 baadaye. Aliandamana na rais katika safari ya kihistoria ya ziara ya kwanza ya first lady nchini China na Umoja wa Kisovyeti, na alikuwa mke wa rais wa kwanza kuteuliwa rasmi kama mwakilishi wa Marekani katika safari zake za peke yake barani Afrika na Amerika Kusini, hali iliyomletea jina la "Bibi Balozi". Pia alikuwa first lady wa kwanza kuingia eneo la vita. Ingawa mumewe alichaguliwa tena kwa kishindo katika uchaguzi wa urais wa mwaka 1972, muda wake kama first lady ulimalizika miaka miwili baadaye, baada ya Rais Nixon kujiuzulu kufuatia kashfa ya Watergate.
Baadaye katika maisha yake, muonekano wake hadharani ulipungua sana. Yeye na mumewe walihamia San Clemente, California, na kisha wakahamia New Jersey. Alipatwa na kiharusi mara mbili, mwaka 1976 na mwaka 1983, na aligunduliwa kuwa na saratan ya mapafu mwaka 1992. Alifariki mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 81.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads